Write & CorrectSwahili
Andika insha ya mfumo wa elimu katika nchi yao
Uingereza watoto wadogo wengi huenda shule za chekechea kabla ya wao huenda shule ya msingi. Watoto wadogo wanaweza kwenda "kikundi cha mchezo ya watoto" wenye umri wa miaka miwili na nusu. Kwa kawaidi watoto wengi huenda shule za chekechea wenye umri miaka mitatu au minne. Ni lazima watoto wote huenda shule wenye umri miaka mitano. Elimu ni bure, lakini baadhi ya wazazi wanalipa kwa shule za binafsi. Baadhi ya shule ni shule za dini lakini wengi sio.
Watoto huenda shule ya msingi kwa miaka sita mpaka wao wenye umri miaka kumi na mimoja. Baada ya shule ya msingi wao huenda shule ya sekondari. Wanafunzi walipofika darasa la kumi na moja, yaani, wenye umri miaka kumi na mitano au kumi na sita, wanafunzi wote hufanya mitihani. Mitihani hii inaitwa G.C.S.E. Kwa Kwaida wanafunzi hufanya mitihani minane au kumi, mara kwa mara wanafunzi wachache wanafanya mitihani kumi na miwili au zaidi. Wanachukua masomo kama baiolojia, jiografia, historia, hesabati, kemia, fizikia, sanaa, muziki na kadhalika.
Baada ya G.C.S.E.'s wanafunzi wengi huendelea masomo yao katika shule kwa miaka miwili zaidi. Wanapofika wenye umri miaka kumi na minane wanafunzi hawa hufanya mitihani tena. Mitihani hii inaitwa A'levels. Kwa kawaida wanafunzi hufanya mitihani mitatu, minne au mitano tu, kama vile, baiolojia, kemia, fizikia na hesabati kama wao wanataka kuwa daktari au mwanasayansi au mhandisi; au fasihi ya kiingereza, lugha, historia, siasa, sanaa au muziki kama wao wanatake kusoma siasa au sanaa katika chuo kikuu. Baadhi ya hutaka kusoma hesabati na sanaa na wengi kuchanganyika masomo katika michanganyiko mengi tofauti. Kuna masomo mengi tofauti kujifunza katika chuo kikuu, kutoka michezo mpaka fizikia ya ulimwengu.
Baada ya wao wanafaulu mitihani yao wanafunzi wanaweza kwenda Chuo kikuu au kazini. Baadhi ya mahali ya kazini panafanya kozi ya mafunzo kwa wanafanyakazi wapya ili waweze kuendelea na elimu yao.